
Suala la Marekani kusitisha msaada latinga bungeni
Dodoma. Baada ya Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kutangaza kusitisha utoaji fedha, Serikali imesema inajiimarisha kuhakikisha inakuza uchumi kwa kutumia vyanzo vya fedha na mapato kujazia maeneo yaliyopungua. USAID imetangaza kusitisha utoaji fedha mpya na usambazaji wa fedha chini ya makubaliano ya malengo ya Maendeleo (DOAGs) hadi uhakiki kwa programu za msaada…