CAG: Sh2.58 bilioni za mikopo ya vijana hatarini kutorejeshwa
Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere amebaini madeni ya mikopo yanayokabiliwa na hatari ya kutorejeshwa ya Sh2.58 bilioni katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Katika aya ya 6.1 ya mwongozo wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana wa Mei 2022, inabainishwa kwamba kipindi cha kurejesha mikopo hakitazidi miezi…