Msigwa aeleza kinachoendelea ukarabati wa Uwanja wa Mkapa, afafanua kuhusu ‘pitch’
Baada ya kujitokeza kwa kasoro ya eneo la kuchezea (Pitch) kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema eneo hilo halikuwa sehemu ya ukarabati unaoendelea. Amesema eneo hilo lilikarabatiwa mwaka 2023 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kwa…