NOTI MPYA KUANZA KUTUMIKA FEBRUARI MOSI, 2025

  Benny Mwaipaja, Dar es Salaam Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emanuel Tutuba amesema kuwa Noti Mpya za Tanzania zenye Saini ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na yeye mwenyewe, za toleo la mwaka 2010, zitaingia kwenye mzunguko kuanzia tarehe mosi Februari mwaka huu. Gavana Tutuba amesema hayo wakati…

Read More

Vijana kutumia vipaji vyao kujiajiri

Unguja. Vijana wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi ili kujiajiri badala ya kutegemea ajira serikalini. Wito huo umetolewa na Balozi wa Vijana Zanzibar, Mohammed Salim Mohammed, Leo Jumatatu Januari 20, 2025, alipotembelea miradi ya kilimo ya Baraza la Vijana Shehia ya Miwani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. Balozi Mohammed amesisitiza…

Read More

Masheha sasa kuhudumia wananchi kidijitali

Unguja. Masheha kisiwani hapa wameanza kutumia mfumo wa kidijitali kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi zaidi na kwa haraka. Mfumo huu, unaojulikana kama eDUA, ni lango kuu la utoaji wa huduma za serikali likilenga kupunguza gharama za matumizi ya karatasi, muda na usumbufu wa kupanga foleni kwa wananchi. Haya yamesemwa leo mjini Unguja na Mkurugenzi…

Read More

Shughuli za binadamu zinavyoharibu Mto Songwe, jitihada za kuunusuru zatajwa

Songwe.  Wahenga waliposema ‘Mchuma janga hula na wakwao’ haukuwa msemo ombwe, hii inajidhihirisha kutokana na zaidi ya watu milioni 1.34 wanaotegemea mto huo wako hatarini kuathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi kutokana na shughuli  za binadamu zinazofanyika pembezoni. Mkazi wa Kijiji cha Magamba akichota maji pembezoni mwa Mto Songwe. Picha na Pelagia Daniel…

Read More

NIKWAMBIE MAMA: Polisi wetu walionaswa kwa rushwa ni kama tone

Siku moja Rais mstaafu wa awamu ya pili, marehemu mzee Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wananchi kuhusu janga la Ukimwi, alijikuta akitamka kwa huzuni kubwa: “Jamani gonjwa hili limekaa kwenye sehemu mbaya…” Binafsi nilimwelewa kuwa gonjwa limekaa kwenye eneo lisiloweza kukwepeka na kiumbe hai. Mfano hewa yote ingegeuka sumu, ni wazi hakuna kiumbe ambaye…

Read More

Wafugaji waitwa kupatiwa chanjo ya kichaa cha mbwa bure

Unguja. Wakati ugonjwa wa kichaa cha mbwa ukitajwa na wataalamu kutokuwa na dawa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeanza kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa bure na kuwataka wamiliki wa wanyama hao kujitokeza kuwachanja ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kupitia Idara ya Maendeleo ya Mifugo, imeeleza kuwa itaendelea kutoa…

Read More

ZFDA yaondoa sokoni vidonge vya PED Zinc kwa kukosa sifa

Unguja. Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA), imeondoa sokoni dawa aina ya PED Zinc (Zinc Sulphate Dispersible Tablet) toleo namba 2203002. Dawa hiyo inatengenezwa na kiwanda cha Beta Healthcare International Ltd cha Nairobi, Kenya. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Januari 21, 2025 na kusainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA, Dk Burhan…

Read More

Wananchi watoa neno ushindi wa Lissu

Moshi. Baadhi ya makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kilimanjaro, wamezungumzia kupatikana kwa safu ya juu ya viongozi wa chama hicho wakisema wanaona mwelekeo mpya.  Hiyo ni baada ya Freeman Mbowe aliyehudumu kama mwenyekiti wa chama hicho kwa zaidi ya miaka 20, kuangushwa na aliyekuwa makamu mwenyekiti wake, Tundu Lissu katika uchaguzi uliokuwa…

Read More

KONA YA FYATU MFYATUZI: Rushwa, najifyatua, nafyatua, tufyatuane

Nachukia rushwa iwe ndogo, kubwa, ya fedha, ngono, vyeo, nk. Zaidi, nawachukia watoaji, wapokeaji, na wanene wanaojifanya kutoiona, hivyo, kutoifyatua. Japo hatuongelei waziwazi, rushwa ni kansa ya kaya. Hivyo, leo, najifyatua, nawafyatyua, na nahimiza tuwafyatue na kufyatuana ili kuikabili, kuifyatua, na kuiondosha rushwa. Japo rushwa hufanyika kisiri, tukifyatuka vilivyo na kuitangazia operesheni na vita kuifyatua…

Read More