
Wawili wafariki dunia kwa kufukiwa mgodini Simiyu
Bariadi. Wachimbaji wadogo wawili wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Ikinabusu namba 2, Wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu, wamefariki dunia baada ya gema kuporomoka na kuwafukia, huku mmoja akinusurika. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto Faustine Mtitu, akizungumza na waandishi wa habari mjini Bariadi, amewataja…