ACT-Wazalendo yasema hakuna kukata tamaa
Dar es Salaam. Licha ya changamoto zinazojitokeza, Chama cha ACT-Wazalendo kimesema mapambano yataendelea na hakuna kukata tamaa. Hayo yamesemwa leo Jumamosi Aprili 12, 2025 mkoani Songwe na kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu katika kongamano la nne la operesheni linda demokrasia lilofanyika mkoani humo. Semu amesema: “Tunawajua maadui wa demokrasia, mtaji wao mkubwa ni hofu…