Haya ndio matumaini mapya wakazi Kisiwa cha Uzi
Unguja. Baada ya kilio, mateso na kuhangaika kwa muda mrefu wakazi wa kisiwa cha Uzi na Ng’ambwa Mkoa wa Kusini Unguja, sasa wameeleza matumaini mapya baada ya kuanza ujenzi wa daraja lenye urefu wa kilometa 2.2 kuunganisha visiwa hivyo na maeneo mengine. Kwa kawaida wananchi wa visiwa hivyo kuingia na kutoka hutegemea kupwa na kujaa…