Wachimbaji wataka kifungu cha sheria ya madini kibadilishwe
Mwanza. Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini nchini wameiomba Serikali kufanya marekebisho au kufuta kabisa Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Madini, Sura ya 123, kinachoruhusu mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji kuingia makubaliano ya msaada wa kiufundi na raia wa kigeni. Wamedai kifungu hicho kimekuwa kikwazo kwao, kwani baadhi ya wageni wanaoingia kwa mwamvuli…