
Watu 15 mbaroni wakidaiwa kuiba mifuko ya unga wa sembe ajalini
Mbeya. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 15, akiwamo Mussa Zacharia (28), mkazi wa Kijiji cha Kanyegere, Wilaya ya Rungwe kwa tuhuma za kuiba mifuko 1,253 ya unga wa sembe iliyokuwa ikisafirishwa kwenda Malawi. Tukio hilo limetokea jana Jumatano, Januari 15, 2025, saa 2:00 asubuhi baada ya lori lenye namba za usajili LA…