M-Bet yatambulisha tovuti yenye huduma bora na bomba kwa wateja

  Na Mwandishi Wetu. Dar es Salaam. Kampuni inayojulikana kwa ubunifu katika sekta ya michezo ya kubahatisha, M-Bet Tanzania, imezindua muonekano mpya wa tovuti yake kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja.  Tovuti hiyo, inayopatikana kupitia www.m-bet.co.tz, inawawezesha wateja kubashiri aina mbalimbali za michezo na kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha kwa urahisi zaidi….

Read More

BARAZA LA SALIM: Jeshi la Polisi Zenji lichunguze vifo tata

Wakati taarifa za kuhimiza amani, utulivu na upendo zikisikika Zanzibar katika nyumba za ibada na kwingineko matukio ya vifo, baadhi vya watu waliokuwa mikononi mwa vyombo vya dola zimeshitua watu na kuuliza visiwa hivi naelekea wapi? Jamaa wa marehemu wawili walioiaga dunia karibuni katika Kijiji cha Kiiungoni, Kusini Pemba, walikataa kupokea maiti hadi sababu ya…

Read More

Watoto wawili waliotoweka wapatikana kwa mganga wa kienyeji

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limesema watoto wawili waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha wakiwa na mfanyakazi wa ndani siku tano zilizopita wamepatikana. Imeelezwa katika taarifa ya polisi kuwa watoto hao wamepatikana wakiwa kwa mganga wa kienyeji Kimara Baruti, jijini Dar es Salaam. Watoto hao, wakazi wa Tandika, jijini Dar es Salaam, ni Husna Gulam…

Read More

Ukosefu wa umeme kikwazo vifaatiba kufanya kazi Chato

Chato. Vifaatiba vyenye thamani ya Sh210 milioni vilivyopelekwa na Serikali katika Kituo cha Afya Nyabilezi, Kata ya Bukome wilayani Chato havitumiki kwa zaidi ya miezi sita. Hali hiyo inatokana na ukosefu wa umeme unaotosheleza kuviwezesha kufanya kazi (umeme wa njia tatu). Kituo hicho kilijengwa kwa gharama ya Sh1.4 bilioni, fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya…

Read More

Trafiki matatani kwa madai ya kudhalilisha Jeshi la Polisi

Dar es Salaam. Askari wa usalama barabarani walioonekana wakichukua rushwa kutoka kwa madereva wa daladala, wamekamatwa na Jeshi la Polisi. Video iliyosambaa mitandaoni leo Januari 15, imewaonyesha askari hao, mmoja wa kike na mwingine wa kiume wakipokea vitu vinavyodhaniwa kuwa fedha kutoka kwa madereva wa daladala zilizosimamishwa na kisha kuwaruhusu waondoke eneo la Vingunguti, Dar…

Read More