
Ukosefu wa umeme kikwazo vifaatiba kufanya kazi Chato
Chato. Vifaatiba vyenye thamani ya Sh210 milioni vilivyopelekwa na Serikali katika Kituo cha Afya Nyabilezi, Kata ya Bukome wilayani Chato havitumiki kwa zaidi ya miezi sita. Hali hiyo inatokana na ukosefu wa umeme unaotosheleza kuviwezesha kufanya kazi (umeme wa njia tatu). Kituo hicho kilijengwa kwa gharama ya Sh1.4 bilioni, fedha za Mpango wa Kunusuru Kaya…