Vilipuzi, baruti kuzalishwa Tanzania | Mwananchi

Kisarawe. Tanzania iko mbio kuacha kuagiza vipulizi na baruti kutoka nje ya nchi. Kila mwaka Tanzania inaagiza vilipuzi milioni 10 na tani 26,000 za baruti kutoka nje. Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema nchi iko mbioni kuachana na uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi. Amesema Kiwanda cha Solar Nitrochemicals Limited kilichozinduliwa leo Jumapili,…

Read More

Mzenji arithi mikoba ya Matata Transit Camp

UONGOZI wa Transit Camp umefikia makubaliano na aliyekuwa Kocha wa Kipanga FC ya visiwani Zanzibar, Ramadhan Ahmada Idd, kukiongoza kikosi hicho kwa michezo iliyosalia, akichukua nafasi ya Stephen Matata aliyeondoka kikosini. Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Ahmada alikiri kufikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo, huku akiomba sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wa…

Read More

Rekodi mbili zambeba Clara Saudia

ZIMESALIA mechi mbili kumalizika kwa Ligi ya Wanawake Saudia, lakini Mtanzania pekee, Clara Luvanga anayekipiga (Al Nassr) ameweka rekodi mbili msimu huu akiwa na kikosi hicho. Nyota huyo wa timu ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars huu ni msimu wa pili tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Dux Lugrono ya Hispania alipocheza miezi mitatu. Al…

Read More

Jela miaka mitano kwa kummwagia mtoto chai ya moto

Geita. Mahakama ya Wilaya ya Geita imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela, pamoja na kulipa faini ya Sh1 milioni baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumjeruhi mtoto mwenye umri wa miaka saba kwa kumwagia chai ya moto. Hukumu hiyo imetolewa Aprili 8, 2025 na Hakimu mwandamizi wa mahakama hiyo, Bruno Bongole baada ya kuridhishwa…

Read More

Jaffar Kibaya aamsha mzuka Mashujaa

MSHAMBULIAJI wa Mashujaa, Jaffar Kibaya anayemiliki mabao matatu hadi sasa katika Ligi Kuu, ametoa hamasa kwa mastaa wenzake hususani wanaocheza eneo la ushambuliaji kutumia kwa makini nafasi wanazozipata ili kuisaidia timu hiyo imalize kibabe mechi zilizobaki ili wasalie kwa msimu ujao. Kibaya aliyeanza kupata nafasi kikosini tangu Mashujaa imuajiri kocha Salum Mayanga aliyewahi kufanya naye…

Read More

Wachezea misitu, wanyooshewa kidole | Mwananchi

Dar es Salaam. Wakati takwimu zikionesha takriban hekta 460,000 za misitu zinapotea nchini kwa mwaka, wanaojihusisha na shughuli za uharibifu ikiwemo kukata miti wameonywa na kutakiwa kuacha tabia hiyo mara moja. Kupotea huko kunasababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo uchomaji moto, ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na mbao zinazofanywa na wenye nia ovu…

Read More

Ukarabati Uwanja wa Ndege Musoma kukamilika Septemba 2025

Musoma. Uwanja wa ndege wa Musoma unaokarabatiwa na kujengwa gharama ya zaidi ya Sh35 bilioni sasa unatarajiwa kukamilika  Septemba mwaka huu baada ya ujenzi huo kushindwa  kukamilika kwa miaka mitatu, kutokana na changamoto mbalimbali ikiwepo ukosefu wa fedha. Awali uwanja huo ulioanza kukarabatiwa na kujengwa Aprili 2021 ulitarajiwa kukamilika Desemba 2022. Mkandarasi anayetekeleza  mradi huo…

Read More

Wabunge CCM mtegoni | Mwananchi

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewatega wabunge wake, baada ya kutangaza mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi hiyo kabla ya kuvunjwa kwa Bunge Juni 27, 2025. CCM imetangaza kufungua pazia la uchukuaji na urejeshaji fomu za ubunge, udiwani na nafasi zote za viti maalumu kuanzia Mei mosi hadi 15, 2025,…

Read More

Vigogo African Sports wala kiapo Championship

KATIKA kuhakikisha African Sports inakwepa janga la kushuka daraja, viongozi wa kikosi hicho wamefanya kikao cha kujadili mambo mbalimbali yanayoihusu, huku kubwa ni jinsi gani ya kukabiliana na ukata wanaokumbana nao kwa sasa. Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa African Sports, Ramadhani Sadiki alisema kutokana na hali wanayopitia waliamua kuitisha kikao na wadau, wanachama na mashabiki…

Read More