
DC Mbozi afariki dunia, akumbukwa kwa uchapakazi
Mbeya/Manyara. Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Mahawe amefariki dunia, viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM), wakimkumbuka kwa uchapakazi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha mkuu huyo wa wilaya kilichotokea leo Januari 14, 2025…