
TMA yatangaza uwepo wa Kimbunga Dikeledi
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa ya uwepo wa Kimbunga Dikeledi katika Bahari ya Hindi mwambao wa pwani ya Msumbiji. Katika taarifa yake, iliyotoa leo Jumanne Januari 14, 2025 mamlaka hiyo inaeleza kuwa, mifumo ya hali ya hewa inaonesha kimbunga hicho kwa sasa kipo mwambao wa pwani ya Msumbiji…