Ajali ya helikopta yaua familia, rubani

New York. Familia ya watu watano kutoka Hispania imefariki dunia katika ajali ya helikopta ya utalii iliyotokea kwenye Mto Hudson, jijini New York, Alhamisi Aprili 10, 2025. Rubani wa helikopta hiyo pia amepoteza maisha. Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Associated Press, waliopoteza maisha ni Agustin Escobar, mtendaji mkuu wa Kampuni ya Siemens Mobility…

Read More

Boti ya Sh4 bilioni kuimarisha uokoaji Ziwa Victoria

Mtwara. Katika jitihada za kupunguza vifo vya wavuvi vinavyotokana na ajali za mara kwa mara katika Ziwa Victoria, Serikali ya Tanzania imepokea boti maalumu ya kisasa ya uokoaji na huduma za matibabu yenye thamani ya Sh4 bilioni. Boti hiyo, ambayo ni sehemu ya makubaliano ya kikanda kati ya Tanzania, Kenya na Uganda, inalenga kuimarisha uwezo…

Read More

Chadema rasmi kutoshiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba

Dodoma. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhani Kailima amesema Chadema ambayo haikusaini kanuni za maadili ya uchaguzi, haitashiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu na chaguzi zote ndogo zitakazofuata kwa muda wa miaka mitano. Kanuni hizo zinasainiwa leo Aprili 12, 2025 na vyama vya siasa vyenye usajili wa…

Read More

Wawili washikiliwa kwa kujifanya askari polisi Geita

Geita.  Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu wawili  kwa tuhuma za kujifanya maofisa polisi na kuchukua kiasi cha Sh25,000 kutoka kwa mwananchi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Saphia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kuwataja kuwa ni Ismail John (25) na Bosco John (28) ambaye ni dereva bodaboda wote wakazi wa…

Read More

Takwimu 5 kali ndani ya rekodi NBA

ARIZONA, MAREKANI: MSIMU mrefu wa NBA 2024-25 unaelekea ukingoni ukiwa umejaa rekodi mpya na matukio ya kukumbukwa. Zikiwa zimesalia saa chache tu kabla ya msimu wa kawaida kufungwa, haya hapa ni mambo matano yaliyovutia macho ya wengi. 1. THUNDER WAMEUPIGA MWINGI Oklahoma City Thunder imeandika historia kwa kuwa timu yenye tofauti kubwa zaidi ya pointi katika…

Read More

RUWASA YAJIBU KILIO CHA UKOSEFU WA MAJI MKOANI PWANI

April 10,2025 Wafugaji wa mifugo mbalimbali ,wametakiwa kuchangamkia fursa ya soko la ndani na nje ya nchi kupitia machinjio ya kisasa ya Union Meat Abattoirs Ltd, yaliyopo katika kijiji cha Kwazoka, Vigwaza, Halmashauri ya Chalinze, mkoani Pwani. Machinjio hayo, ambayo yamegharimu zaidi ya sh.bilioni 26, huzalisha bidhaa za nyama zinazouzwa ndani ya Tanzania na kusafirishwa…

Read More

Mbinu za jamii kukwepa sheria ndoa za utotoni-2

Meatu. Licha ya Tanzania kuwa na sheria zinazozuia ndoa na mimba za utotoni, jamii inatumia usiri na uongo kama mbinu ya kuepuka mkono wa sheria. Mbali ya hayo, Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inatajwa kuchochea hali hiyo kwa kuwa inaruhusu wasichana kuolewa wakiwa na miaka 14 kwa idhini ya mahakama na miaka 15 kwa…

Read More

Chadema kwenye mtego mwingine kanuni za maadili

Dar es Salaam. Tusaini au tusisaini? ndilo swali lisilo na jawabu ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa sasa, kuhusu ushiriki wake katika kujadili na kusaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kesho Aprili 12, 2025. Kanuni za maadili zimeandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 162 (1), (2) na…

Read More