
Vijumbe wa upatu na mzigo wa madeni kwa sio waaminifu
Dar es Salaam. Inaelezwa viongozi wengi wanaoongoza vikundi vya upatu wanakutana na changamoto kubwa ya madeni baada ya washiriki kushindwa kulipa fedha kwa wakati, kuchelewesha, au hata kutoweka bila taarifa. Hali hii imeathiri hasa upatu unaochezeshwa mtandaoni, ambapo baadhi ya wanufaika huzima simu, kuhama makazi, na hata kutoweka, jambo linalowaweka viongozi wa upatu kwenye matatizo….