Majeruhi ajali ya Msoga waruhusiwa

Bagamoyo. Majeruhi wote 21 waliokuwa wamelazwa kwenye Hospitali ya Msoga Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kufuatia ajali iliyohusisha Coaster na lori wameruhusiwa baada ya afya zao kutengamaa. Ajali hiyo iliyotokea Januari 10, 2025 Kijiji cha Mazizi Mkoani Pwani inadaiwa kusababishwa na uzembe wa dereva wa Coaster aliyekuwa anaendesha gari huku akitumia…

Read More

Serikali kuanza kuandaa wauguzi na wakunga bobezi

Arusha. Katika kukuza utalii wa matibabu na kufikia malengo ya kitaifa ya kutokomeza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua, Serikali inatarajia kuanza kuwasomesha wauguzi na wakunga katika masomo ya ubingwa na ubingwa bobezi. Hayo yamesemwa leo Januari 11,2025 jijini Arusha na Waziri wa Afya Jenista Mhagama wakati akikagua na kuzindua chumba cha huduma za dharura…

Read More

Kituo cha afya Chifutuka chapata gari la kubebea wagonjwa

Bahi. Wananchi wapatao 18,604 wa Kata ya Chifutuka wameishukuru Serikali kwa hatua ya kuwaletea gari la kubebea wagonjwa ambalo litahudumu kwenye kituo cha afya Chifutuka ambacho pia kinahudumia wananchi kutoka Wilaya ya Singida Vijijini mkoa wa Singida. Wakizungumza leo Jumamosi, Januari 11, 2025 wakati wa makabidhiano hayo na Mbunge wa wilaya ya Bahi Kenneth Nollo,…

Read More

1,675 watibiwa magonjwa ya ngono Njombe

Njombe. Kaimu Mganga mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk David Ntahindwa amesema mwaka 2024 huduma ya uzazi wa mpango ilitolewa kwa vijana balehe wapatao 35,223 (wenye umri kati ya miaka 10 hadi 24) huku zaidi ya 1,600 wakitibiwa magonjwa ya ngono. Takwimu hizo zimetolewa leo Januari 11, 2025 wakati wa mkutano wa Naibu Waziri Ofisi…

Read More

200,000 wajitokeza kuomba ajira 14,648 za ualimu

Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema usaili wa walioomba ajira kwenye kada ya ualimu utafanyika kuanzia Januari 14 hadi Februari 24 mwaka huu kwenye vituo vya usaili vilivyopo kwenye mikoa ambayo wasailiwa hao wanaishi. Simbachawene amesema nafasi za ualimu zilizotangazwa na Serikali ni 14,648 lakini…

Read More

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA AFRIKA KUHUSU KILIMO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 11, 2025 ameshiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mpango wa Maendeleo ya Kilimo Afrika ambapo alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Speke Resort, Munyonyo, Kampala Uganda. Awali Mheshimiwa Majaliwa alishuhudia Tamasha la…

Read More