RPC Jongo: Msikubali kukamatwa na askari asiye na kitambulisho

Geita. Jeshi la Polisi mkoani Geita limetoa wito kwa wananchi kutokubali kukamatwa na mtu yeyote anayejitambulisha kama askari polisi bila kuonyesha kitambulisho cha utumishi na kueleza kituo cha polisi alichotoka. Jeshi hilo limesema kitendo cha kutokuonyesha kitambulisho au kituo cha kazi ni kinyume cha sheria na kinaweza kutumika kama mbinu ya kuficha vitendo vya kihalifu….

Read More

Majaliwa: Viongozi wa dini himizeni amani wakati wa uchaguzi

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa dini, vyama vya siasa na mashirika yasiyo ya kiserikali, kuhamasisha wananchi wazingatie amani na utulivu wakati wa uchaguzi. Ametaka hilo liambatane na kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kuwachagua viongozi. Majaliwa anakuja na kauli hiyo katika kipindi ambacho, Chama cha…

Read More

Jela kwa kubaka na kumpa mimba mwanafunzi

Mwanza. Mahakama ya Wilaya ya Kwimba, mkoani Mwanza, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela mkazi wa Kijiji cha Kinamweli, Iddy Makungu (30) kwa kosa la kubaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 14. Hukumu hiyo imetolewa jana Jumanne Aprili 8, 2025 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ndeko Dastan Ndeko, ambaye amesema mtuhumiwa…

Read More

Ushirikiano wa THBUB na DIHR Watengeneza Uelewa Juu ya Haki za Binadamu kwa Wavuvi Wadogo

 Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Patience Ntwina akizungumza leo Aprili 09, 2025 wakati akifungua mafunzo muhimu kwa watumishi wa Tume kuhusu usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za bahari kwa wavuvi wadogo wadogo sambamba na kuzingatia haki za binadamu. Mafunzo haya yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Four Points…

Read More

Aliyeua ndugu watatu, ahukumiwa kunyongwa hadi kufa

Arusha.”Ni mauaji ya kusikitisha.” Ndivyo unavyoweza kusema baada ndugu watatu ambao Ester Matei, Lidia Matei na Anjela Barnaba kuuawa kwa kuchomwa visu sehemu mbalimbali za miili yao. Mauaji hayo yalitokea Septemba 18, 2022 katika Kijiji cha Mchangani ambapo Anjela (marehemu) alikwenda kufanya usafi kwenye kaburi la baba yake akiongozana na watoto wa ndugu zake Ester…

Read More

Kupaa kwa bei ya samaki kwamwibua mbunge, ajibiwa

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema mapendekezo ya kupunguza tozo na kodi za uingizaji wa samaki kutoka nje ya nchi yatafanywa kulingana na matokeo ya tathmini itakayofanywa na Kamati ya Maboresho ya Mfumo wa Kodi. Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande ameyasema hayo leo Jumatano Aprili 9, 2025 wakati akijibu swali la msingi la Mbunge…

Read More