Madereva wa Serikali watajwa vinara wa ‘ku-ovateki’, spidi
Dar es Salaam. Baraka Ludohela (32), ambaye amefungiwa leseni ya udereva kwa miezi mitatu, ni miongoni mwa madereva wa magari ya Serikali wanaotajwa kukaidi sheria za usalama barabarani. Madereva hao wanalaumiwa kwa kuendesha kwa mwendo kasi, kuyapita magari mengine bila tahadhari na kutotii maagizo ya askari wa usalama barabarani. Inadaiwa kuwa baadhi yao hukingiwa kifua…