Lissu: Tutaandamana siku ya uchaguzi kuuzuia

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike. Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya ‘No Reforms, No Election’ (bila mabadiliko,…

Read More

Barabara Somanga – Mtama kula kichwa cha mtu Tanroads

Lindi. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa wataalamu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), waliokwamisha kwa uzembe urejeshaji wa mawasiliano katika barabara kuu ya Dar es Salaam–Lindi, eneo la Somanga Mtama mkoani Lindi. Akizungumza baada ya kukagua kazi za urejeshaji wa mawasiliano yaliyokatika tangu Aprili 6, 2025, Waziri Ulega amesema…

Read More

Wakimbiaji 700 kushiriki Fistula Marathon Arusha

Wanariadha wa kimataifa, Failuna Abdi Matanga na Angelina John, wamejitosa kuwa mabalozi wa mbio za Fistula Marathon zinazolenga kusaidia matibabu ya wanawake wanaoathirika na ugonjwa huo wakati wa kujifungua. Mbio hizo kwa msimu wa nne zinatarajia kufanyika Mei 25, 2025 jijini Arusha zikishirikisha wakimbiaji zaidi ya 700 ikiwa ni kwa ajili ya kusaidia utoaji elimu…

Read More

Aliyewahi kuwa RPC Kilimanjaro afariki duniani

Moshi. Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Absalom Mwakyoma amefariki dunia leo April 7, 2025 mkoani hapa baada ya kuugua ghafla. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo, April 7, 2025 akisema amefariki njiani akipelekwa Hospitali ya KCMC. “Kifo chake kimetokea leo Aprili 7, 2025…

Read More

Wahudumu wa afya waonywa lugha chafu kwa wagonjwa Mbeya

Mbeya. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Elizabeth Nyema ametoa angalizo kwa watoa huduma kwenye hospitali za Serikali, vituo vya afya na zahanati kuepuka matumizi ya lugha chafu za kukatisha tamaa  kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma. Hatua hiyo imetajwa kusababisha malalamiko ya wananchi jambo linalowafanya kuona vituo vya afya sio  kimbilio la kupata huduma bora…

Read More

EAC kuanzisha kituo cha onyo kudhibiti mauaji ya halaiki

Arusha. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeanza mchakato wa kuanzisha Kituo cha Onyo la Mapema, kitakachofanya kazi ya kulinda amani na utulivu katika nchi zote wanachama na kuzuia mauaji ya halaiki. Hayo yamesemwa leo Aprili 7,2025 jijini Arusha na Katibu Mkuu wa EAC, Veronica Nduva, kwenye maadhimisho ya miaka 31 tangu kutokea kwa mauaji ya…

Read More

Chaumma yashauri marekebisho Tume ya Uchaguzi

Mbeya. Pamoja na kuthibitisha kushiriki uchaguzi mkuu wa 2025, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma) kimependekeza na kuishauri Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) baadhi ya mambo ya kufanyiwa marekebisho kabla ya shughuli hiyo. Tanzania inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Oktoba 25, 2025 kuwapata madiwani, wabunge na Rais huku chama hicho kikitarajia kusimamisha wagombea katika…

Read More