
Kituo kikubwa kujaza gesi kwenye magari UDSM kuanza kazi
Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dk James Mataragio amesema kituo cha kujaza gesi asilia kwenye magari eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kitaanza majaribio ya awali Januari 16, 2025. Amesema kituo hicho chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kilipaswa kuanza kazi Desemba 2024, lakini kimechelewa…