Wakulima waiangukia Serikali kuondoa kodi kwenye mifuko
Dodoma. Wakati maandalizi ya bajeti ya mwaka 2025/26 yakiendelea, wakulima wameiangukia Serikali kuweka ruzuku au kupunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mifuko ‘kinga njaa’ (hermetic storage bags) kwenye bajeti hiyo, ili kuwaepusha na hasara inayotokana na upotevu wa mazao baada ya mavuno. Mfuko mmoja unauzwa kati ya Sh5,000 hadi 5,500, hivyo imekuwa kikwazo…