
Mwenyekiti UWT Njombe arudisha tabasamu kwa mlemavu wa viungo wilayani Wanging’ombe
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe Dkt.Scholastika Kevela ameitumia sikukuu ya mwaka mpya kurudisha tabasamu usoni kwa Amir Mtendwa mwenye ulemavu wa kupooza miguu. Mtendwa ambaye ni mkazi wa Kata ya Uhenga wilayani Wanging’ombe amekuwa akiendelea kutaabika kutokana na hali yake ya ulemavu wa miguu…