
Utafutaji watoto wa jinsi fulani unavyovuruga familia
Dar es Salaam. Mume amechepuka. Mchepuko ameshika ujauzito, hatimaye mtoto wa kiume amezaliwa. Ni mume wa mke aliyefunga naye pingu za maisha miongo mitatu iliyopita na kujaaliwa watoto wanne wote wa kike. Hatimaye siri imefichuka. Mke na watoto wamejua kwamba baba ana mtoto nje ya ndoa na familia imegeuka tanuru la moto. Mume analaumiwa kwa…