
Daraja lililovunjika Same kujengwa usiku na mchana
Same. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewataka wataalamu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) wanaojenga Daraja la Mpirani wilayani Same kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linakamilika ndani ya siku tatu. Daraja hilo lililopo Kijiji cha Mpirani, Kata ya Maore, lilivunjika Januari 2, 2025 baada ya nguzo kuathiriwa na maji ya mvua. Kuvunjika kwa daraja…