MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AMLILIA JAJI WEREMA

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari ameshiriki mazishi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mstaafu Frederick Werema, yaliyofanyika tarehe 04 Januari, 2025 katika Kijiji cha Kongoto, Wilayani Butiama Mkoani Mara. Akizungumza wakati wa utoaji wa Salamu za Pole, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, amesema kuwa Jaji Werema alijitolea kwa hali na mali…

Read More

Jaji Mkuu aongoza maziko ya Werema, azungumzia mchango wake

Butiama. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma ameongoza mamia ya watu katika mazishi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Frederick Werema katika mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Kongoto kilichopo Wilaya ya Butiama mkoani Mara. Jaji Werema (69) alifariki dunia Desemba 30, 2024 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada…

Read More

ULEGA ATAKA WAZAWA WAPEWE KIPAUMBELE UJENZI WA BARABARA

Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega amewataka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kuhakikisha unatoa kipaumbele kwa vijana wazawa katika ujenzi wa miradi ya barabara inayoendelea nchini ili kupata ajira, kukuza ujuzi na uchumi kwa watanzania. Akizungumza na wananchi wa Kata ya Ndungu wilayani Same katika hafla ya kumkabidhi Mkandarasi China Communication Construction Company (CCCC), anayejenga barabara…

Read More

Rufaa yawapa wanne ahueni ya adhabu

Arusha. Mahakama ya Rufani imempunguzia adhabu Amedeus Kavishe kutoka malipo ya faini ya Sh1.077 bilioni au kifungo cha miaka 20 jela aliyohukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kukutwa na nyara za Serikali na risasi kinyume cha sheria hadi faini ya Sh27.6 milioni. Mahakama hiyo iliyoketi Moshi imempunguzia adhabu baada ya kumuondolea hatia katika mashtaka mengine…

Read More

RAIS WA ZANZIBAR AFUNGUA SKULI YA SEKONDARI YA KWANZA TUMBATU IKIWA NI SHAMRASHAMRA ZA MIAKA 61 YA MAPINDUZI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika tabasamu wakati akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Zanzibar Mhe. Haji Omar Kheri, wakati akielekea katika eneo la ufunguzi wa Skuli ya Sekondari Tumbatu, ufunguzi wa Skuli hiyo uliofanyika leo 4-1-2025, ikiwa ni Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 61…

Read More

Yanga yamshusha staa mpya Kwa Mkapa

YANGA ikiwa inapambana uwanjani leo jioni ikiizamisha TP Mazembe kwea mabao 3-1, jukwaani akaonekana mshambuliaji mpya, Jonathan Ikangalombo, ambaye Mwanaspoti liliwaripotia kwamba yupo hatua ya mwisho kumalizana na klabu hiyo ya Jangwani. Ikangalombo anyemudu kucheza winga zote mbili anayetokea AS Vita alionekana jukwaa Kuu la VVIP akiwa na maofisa wa Yanga wakithibitisha wazi kwamba yupo…

Read More

Straika Coastal Union atwishwa zigo

KOCHA wa Coastal Union, Juma Mwambusi amesema mshambuliaji mpya wa kikosi hicho raia wa Mali, Amara Bagayoko atakuwa na msimu bora ndani ya timu hiyo kutokana na uwezo alionao, licha ya kutopata muda mwingi wa kucheza kikosini. Nyota huyo ametambulishwa katika dirisha hili dogo la usajili, japokuwa Mwanaspoti linatambua Bagayoko alikuwa na timu hiyo tangu…

Read More