Wataalamu waeleza umuhimu wa kubadilisha shuka kila baada ya wiki moja
Dar es Salaam. “Kufua shuka mpaka nione linabadilika rangi, kitu pekee ninachoheshimu ni foronya ya mto hiyo baada ya siku kadhaa huwa nahisi inatoa harufu, kwa kuwa huchafuka haraka kuliko shuka,” hiyo ni kauli ya kijana Omary Juma, akielezea anabadilisha shuka baada ya siku ngapi. “Nakumbuka nikiwa shule tulilalia mashuka mpaka siku ukifua unalala usingizi…