Lissu ahoji mashahidi wake kuwekwa kando
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu ameibuka na mapya akiilalamikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, pamoja na mambo mengine kwa kutokuorodhesha mashahidi anaokusudia kuwaita mahakamani katika kesi ya uhaini inayomkabili. Miongoni mwa mashahidi aliodai aliwataja lakini hawakuorodheshwa ni Samia Suluhu Hassan, Dk Philip Mpango na Kassim Majaliwa. Lissu…