Taasisi za Ulinzi wa Mlaji zimetakiwa kushirikiana na FCC
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleimani Jafo, amezitaka taasisi zote za serikali zinazohusika na ulinzi wa mlaji kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha haki za watumiaji zinalindwa. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Haki za Watumiaji Duniani, Dkt. Jafo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mamlaka mbalimbali za udhibiti…