Afrika Kusini yatoa mshindi wa Sh30 milioni mashindano ya Quran
Unguja. Wakati yakifanyika mashindano ya kuhifadhi Quran kwa Afrika, Mohamed Amejair (23) kutoka Afrika Kusini ameibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha Sh30 milioni, huku Rais Hussein Mwinyi akisema yanaitangaza Zanzibar kimataifa. Mashindano hayo yamefanyika leo Machi 22, 2025 katika Uwanja wa Aman Complex, Unguja mgeni rasmi akiwa Dk Mwinyi. Yamewashirikisha vijana 10 waliohifadhi Quran juzuu…