
Mwaka 2025 waanza kwa kicheko, mafuta yakishuka bei
Dar es Salaam. Bei ya petroli na dizeli ya rejareja kwa Januari 2025 imeendelea kushuka nchini, ikilinganishwa na Desemba 2024, huku sababu kubwa ikitajwa ni kupungua kwa viwango vya kubadilishia fedha za kigeni. Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaonyesha bei za mafuta kuanzia leo Jumatano Januari 1,…