Tanesco kuokoa mabilioni iliyotumia kukodi vitendea kazi
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limetangaza kuokoa Sh1.3 bilioni kila mwezi, zilizokuwa zikitumika kukodi vitendea kazi vinavyotumika kwenda kuwahudumia Watanzania katika mwaka wa fedha 2024/25. Kutokana na gharama hiyo, shirika limenunua bajaji 100, magari 100 na pikipiki 284 ambazo tayari zimeanza kugawiwa katika ofisi za mikoa na wilaya za Tanesco kote nchini…