
Vikosi vya SMZ vyaanzisha miradi kujiongezea mapato
Unguja. Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Rahma Kassim Ali amesema ujenzi wa miradi unaofaywa na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) utawezesha mapato kupatikana na kutatua mahitaji ya msingi bila kusubiri mgawanyo wa fedha za bajeti. Amesema fedha za bajeti zinasubiriwa na wengi na haziwezi kumaliza mipango ya vikosi hivyo, kwani…