Putin akubali kusitisha mapigano Ukraine, atoa masharti matatu

Rais wa Russia, Vladimir Putin amekubali kwa kanuni pendekezo la kusitisha mapigano nchini Ukraine kwa muda wa siku 30 lililowasilishwa na Marekani, lakini ameweka masharti kadhaa. Amesisitiza kuwa vipengele muhimu vinahitaji kujadiliwa zaidi ili kuhakikisha amani ya kudumu. Masharti yaliyotolewa na Putin ni pamoja na Ukraine kutotumia kipindi cha kusitisha mapigano kujihami upya au kupokea…

Read More

Usichokijua kuhusu ulaji wa uyoga na maajabu yake

Dar es Salam. Uyoga  ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba na protini ambayo hufanya vizuri katika mwilini wa binadamu. Kama ulikuwa hufahamu uyoga una nyuzi nyuzi nyingi na hauna mafuta  na chumvi ya sodium. Mtaalamu wa Sayansi na Teknolojia ya Chakula, Francis Modaha, anasema uyoga una kundi la vitamini B kwa wingi, yaani vitamini B2  (Riboflavin), Niacin na Pantothenic acid. Anasema…

Read More

Usichofahamu kuhusu waziri wa kwanza mwanamke Tanzania

Imeandikwa na Mzee wa Atikali: Buriani mama yangu mkubwa Tabitha Siwale, waziri wa kwanza mwanamke “Mama Tabitha Siwale became Tanzania’s first female Minister in 1975”. Prof. M. Mwandosya, Jan. 20, 2014. “Pole sana Ganga. Hiki ni kilio chetu sote tuliomfahamu Mama Siwale na Taifa pia. Mama Siwale alifungua njia za uhuru wa wanawake kujieleza na…

Read More

Kichocheo ukuaji uchumi Tanzania chatajwa

Arusha. Uwajibikaji na uwazi katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia Tanzania, unatajwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza imani ya wananchi kwa Serikali kuhusu namna rasilimali zinavyowanufaisha. Pia, Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili rasilimali hizo ziweze kuinua uchumi kuanzia wa mtu binafsi hadi Taifa kwa ujumla. Waziri wa Mambo…

Read More

Aishi Manula kuna nini? | Mwanaspoti

YUKO wapi Manula? Kuna nini kinaendelea? Ni maswali yanayosumbua kwa sasa vichwani mwa mashabiki wa soka baada ya kipa huyo tegemeo wa timu ya Taifa kutoonekana uwanjani kwa muda mrefu. Baada ya kuwepo kwa tetesi za kipa Moussa Camara kuumia katika mechi dhidi ya Azam, wengi waliamini ilikuwa nafasi ya Manula kurudi langoni. Hata hivyo,…

Read More

Hii hapa tiba ya figo zilizofeli

Figo ni kiungo muhimu sana mwilini. Mungu ametupa figo mbili moja kulia na nyingine kushoto, ziko tumboni chini ya mbavu. Figo huanza kazi tangu mtoto akiwa tumboni mwa mama yake. Kazi ya figo ni kuchuja damu, kuondoa taka mwili, kudhibiti uwiano wa madini na maji mwilini. Figo pia husaidia mchakato wa kutengemeza damu na kuimarisha…

Read More

Nurdin Bakari ashtukia jambo Bara

BEKI wa zamani wa Simba, Yanga na Taifa Stars, Nurdin Bakari amesema amekuwa akiifuatilia kwa ukaribu Ligi Kuu ya msimu huu na kubaini kuna uwezekano mkubwa yale yaliyojitokeza msimu wa 2016-2017 yakajirudia kwa bingwa kuchukua ubingwa kwa tofauti ya uwiano wa mabao. Nurdin aliliambia Mwanaspoti kwamba hadi sasa ni ngumu kutabiri timu ipi itabeba ubingwa…

Read More

KONA YA WASTAAFU: Nyongeza ya Pensheni ya wastaafu inapooteshwa mbawa!

Oktoba 2024, iliyopita, siri-kali ilijikanyaga katika kile ilichookita ni kumsaidia mstaafu wake wa Kima cha Chizi kuweza kukabiliana na hali ngumu ya maisha iliyokuwa ikimkabili. Ilimtangazia mstaafu huyo nyongeza ya pensheni ya Sh50,000 ambayo ukiongeza na ile laki moja kwa mwezi aliyokuwa akipata kwa miaka 21 nyuma, angekuwa sasa akipata Sh150,000. Siri-kali haikulazimishwa na yoyote….

Read More

Nyoni agoma kushuka daraja | Mwanaspoti

NYOTA wa kimataifa wa Tanzania anayeshikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars, Erasto Nyoni anayeitumikia Namungo kwa sasa, amekataa kushuka na timu hiyo akisema licha ya kuwa na hali mbaya msimu huu, lakini bado wana nafasi ya kujisahihisha. Namungo iliyopanda daraja msimu wa 2019-2020 kwa sasa ipo nafasi ya…

Read More

Unene bado janga kwa wakazi wa mijini

Dar es Salaam. Kutokana na utafiti kubaini wakazi wa mijini kuwa na unene kupita kiasi ikilinganishwa waishio vijijini, wataalamu wa lishe na afya ya binadamu wameeleza aina ya maisha wanayopaswa kuishi wakazi wa mijini. Wataalamu hao wanaeleza hayo wakati uhalisia wa maisha ya wakazi wa mijini yakionyeshwa kwenye Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi…

Read More