
Serikali kuanza kuandaa wauguzi na wakunga bobezi
Arusha. Katika kukuza utalii wa matibabu na kufikia malengo ya kitaifa ya kutokomeza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua, Serikali inatarajia kuanza kuwasomesha wauguzi na wakunga katika masomo ya ubingwa na ubingwa bobezi. Hayo yamesemwa leo Januari 11,2025 jijini Arusha na Waziri wa Afya Jenista Mhagama wakati akikagua na kuzindua chumba cha huduma za dharura…