
Simulizi ya aliyetolewa uvimbe wa kilo tano kwenye mfuko wa mayai
Dar es Salaam. Mama mwenye umri wa miaka 52 (jina limehifadhiwa), mkazi wa Bagamoyo mkoani Pwani, amepitia changamoto kubwa ya kiafya baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kilo 5.5 uliokuwa kwenye mfuko wake wa mayai. Mama huyo akizungumza na Mwananchi, ameeleza namna alivyogundua tatizo hilo, ambalo anasema lilimuanza Agosti, 2024 na kumsababishia maumivu…