WADAU WANAKUJA NA MIKAKATI YA KUHAMASISHA WASICHANA NA WANAWAKE WENYE ULEMAVU KUSHIRIKI MICHEZO
Na Nihifadhi Abdulla KATIKA jamii nyingi, wanawake wenye ulemavu wanakumbwa na changamoto nyingi zinazowazuia kushiriki katika michezo. Pamoja na uwepo wa mikataba ya kimataifa kuhusu haki za binadamu, bado kuna uelewa mdogo kuhusu nafasi ya wanawake wenye ulemavu katika sekta ya michezo. Miongoni mwa changamoto kubwa zinazotajwa kuathiri ushiriki wao ni mitazamo potofu ya jamii…