Anasa zamponza Rais mstaafu Georgia, atupwa jela miaka tisa
Thibilisi. Rais wa zamani wa Georgia, Mikhail Saakashvili amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela kwa ubadhirifu wa mali ya Umma. Mamlaka za Georgia zilimkamata Saakashvili Oktoba 2021 alipoingia kwa siri nchini humo akitokea uhamishoni Ukraine wakati wa uchaguzi na kumshutumu rais huyo wa zamani kwa matumizi mabaya ya madaraka, ubadhirifu wa fedha na makosa mengine…