AKILI ZA KIJIWENI: Kama vipi, viwanja vyote korofi wapewe JKT
TFF sasa hivi imekuwa haina masihara na viwanja ambavyo vinashindwa kutimiza vigezo vya kutumika kwa ligi ambapo inavitembezea hasa rungu pasipo kutanguliza mambo ya busara. Na hiki ndicho ambacho sisi hapa kijiweni tulikuwa tunatamani kitokee kwamba kama viwanja havifanyiwi ukarabati basi timu zinazovitumia zionje shubiri ya kucheza mechi zao za nyumbani kwingineko. Visipokuwa vinapewa adhabu…