Mmoja afariki, 33 wajeruhiwa ajali ya Coaster na katapila
Songwe. Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 33 kujeruhiwa katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Coaster lililogongana na katapila, iliyotokea jana mchana eneo la Msinde Wilaya Momba mkoani Songwe. Kamanda wa Polisi mkoani Songwe, Augustino Senga amesema ajali hiyo imetokea jana Machi 10, 2025 saa sita mchana ikihusisha gari aina ya Toyota Coaster…