
Bodaboda wamchangia Samia Sh1 milioni za kuchukua fomu
Tanga. Wanachama wa Umoja wa Wamiliki wa Waendesha Pikipiki na Bajaji Wilaya ya Tanga (Uwapibata) wamechanga Sh1 milioni kwa ajili ya Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua fomu ya kugombea urais kwa mwaka 2025. Fedha hizo wamezikabidhi leo Januari 4, 2025, wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, jijini hapa….