
Simulizi hukumu kesi ya Sanga wa Chadema na wenzake- 1
Njombe. Haki imetendeka. Hii ndio kauli inayosikika vinywani mwa makada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya wenzao, George Sanga na wenzake wawili, kuachiwa huru kwa tuhuma za mauaji. Hii ni baada ya kukaa mahabusu siku 1,557 tangu walipokamatwa Septemba 26, 2020 kwa tuhuma za mauaji ya kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM),…