Simba yaichapa TMA, yafuzu 16 bora

SIMBA imetinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho (FA) kufuatia kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TMA Stars kwenye mchezo uliochezwa  Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, leo, ambapo sasa inakwenda kucheza dhidi ya Big Man. Ndani ya dakika 45 za kipindi cha kwanza, Simba ilionekana kutawala huku ikisukuma mashambulizi…

Read More

Mwarobaini watu wenye ulemavu kubaguliwa kwenye ajira wasakwa

Dar es Salaam. Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO) limetaja vikwazo vitatu wanavyokumbana navyo watu wenye ulemavu wanaposaka ajira, huku mtandao uwezeshaji wa wenye ulemavu mahali pa kazi ukitajwa ni mwarobaini wa changamoto za ajira kwa kundi hilo. Vikwazo vinavyotajwa kuwakumba wenye ulemavu wanaposaka fursa za ajira ni mtazamo na mazingira. Hayo yameelezwa…

Read More

Minziro akalia kuti kavu Pamba JIji

KOCHA wa Pamba Jiji, Fred Felix ‘Minziro’, amejikuta kwenye presha kubwa kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mechi mbili zilizopita za ligi, hali inayochochea madai baadhi ya wachezaji wake hasa wa kigeni wanashindwa kuelewa mbinu zake za kiufundi.  Minziro ambaye alichukua nafasi ya Goran Kopunovic Oktoba 2024, amepewa muda mfupi kubadili mambo katika…

Read More

Serikali kutumia Sh57 trilioni mwaka ujao wa fedha

Dodoma. Mwelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2025/2026 imeonyesha ongezeko la asilimia 13, ikikua kutoka Sh50.29 trilioni katika mwaka wa fedha 2024/25 hadi kufikia Sh57.04 trilioni, ikiwa na vipaumbele sita. Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/25 ilikuwa Sh49.34 trilioni. Hata hivyo, Februari 14, 2025 Bunge lilipitisha bajeti ya nyongeza ya jumla ya…

Read More

Wadau wakutana kujadili rasimu ya maendeleo

Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) limekutana na wadau mbalimbali ili kupokea maoni ya rasimu ya maendeleo ya viwanda yatakayowezesha kufikia malengo, shabaha na kutekeleza mikakati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini. Baadhi ya maoni yaliyopokelewa  kwenye kikao hicho ni pamoja na masuala ya umeme, malighafi, teknolojia, kodi na rasilimali watu. Akizungumza…

Read More

Mbeya yaanza mchakato kuligawa jimbo la Dk Tulia

Mbeya. Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuchunguza na kuligawa Jimbo la Mbeya Mjini kupata jimbo jipya la Uyole, katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2025. Mchakato huo ukikamilika na kukidhi vigezo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) italitangaza jimbo jipya, jambo ambalo litakuwa jawabu la matakwa ya wakazi wa Mbeya Mjini….

Read More

KONGAMANO LA TATHIMINI YA UJENZI WA HOSPITALI YENYE MAADILI YA KIISLAMU LAFANYIKA TANGA

Na Oscar Assenga, TANGA KONGAMANO la Tathimini ya Ujenzi wa Hospitali itakayosimamia maadili ya Kiislamu limefanyika Jijini Tanga huku wadau wa maendeleo nchini wakiombwa kuchangia kufanikisha ujenzi huo ambao utakuwa chachu kwa kutoa huduma kwa maadili ya kiislamu.Akizungumza wakati wa kongamano hilo Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanga Islamic Development Foundation (TIDF) ujenzi wa Hospitali hiyo…

Read More

Beki Azam atua Ulaya | Mwanaspoti

BEKI wa kushoto raia wa Senegal, Cheick Sidibe amejiunga na klabu ya HJK Helsinki ya Finland akiwa mchezaji huru baada ya kuachana na matajiri wa Chamazi, Azam FC. Usajili huu unamfanya Sidibe kuwa mchezaji mpya wa kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu ya Finland, maarufu kama Veikkausliiga.  Sidibe amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu hiyo,…

Read More

Jela miaka mitano kwa wizi wa nguruwe

Simiyu. Washtakiwa wawili kila mmoja amefungwa miaka mitano jela kwa wizi wa nguruwe. Waliokumbwa na adhabu hiyo katika Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ni Masunga Chenya(20)na Daud Elias(19) wakazi wa Mtaa wa Sola mjini Maswa. Kabla ya hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Aziz Khamis kutoa hukumu hiyo leo Jumanne Machi 11,2025, Mwendesha mashitaka…

Read More