Yanga, Simba yaahirishwa, kupangiwa tarehe nyingine
Mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga na Simba iliyokuwa imepangwa kuchezwa leo Jumamosi Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa imeahirishwa rasmi na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB). Uamuzi huu umetokana na sintofahamu iliyotokea baada ya klabu ya Simba kuzuiwa kuingia uwanjani kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo huo,…