
Moto wateketeza mali za wapangaji, Sh3.4 milioni
Moshi. Moto ambao chanzo chake hakijajulikana umeteketeza vyumba vitatu vya wapangaji katika Mtaa wa Wailesi, Kata ya Soweto, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro wakati wakijiandaa kupika chakula cha mchana kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya 2025. Vyumba hivyo vitatu vimeteketea kwa moto leo , Januari Mosi, 2025 ambapo kaya tatu kwa sasa hazina mahali pa kuishi…