
Mchungaji Mpambichile ‘awachorea ramani’ waumini kufikia mafanikio 2025
Kibaha. Mchungaji wa Kanisa Anglikana la Mtakatifu Gabriel, Kibaha Pwani, Exavia Mpambichile amewahamasisha waumini wake kuanza mwaka mpya wakiwa na malengo thabiti ya maendeleo, hasa katika sekta ya uchumi. Akizungumza katika ibada ya mkesha wa mwaka mpya iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Januari Mosi, 2025 kwenye kanisa hilo, Mpambichile alisisitiza umuhimu wa kuwa na malengo…