Maswali tata ‘No Reforms, No Election’ ya Chadema
Dar es Salaam. Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiweka msimamo wa kuzuia uchaguzi mkuu ujao endapo mabadiliko wanayoyataka hayatafanyika, mchambuzi wa siasa na mwanaharakati wa maendeleo, Ansbert Ngurumo amehoji maswali manne kwa Chadema na wafuasi wao. Ngurumo ambaye pia ni mwanahabari mkongwe, anahoji hatma ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini endapo kaulimbiu…