Vikundi 60 vyalamba mkopo Sh1.13 bilioni Ilemela, vyaonywa ‘kuponda maisha’
Mwanza. Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imetoa mkopo wa Sh1.13 bilioni kwa vikundi 60, huku Serikali ikionya dhidi ya matumizi yasiyofaa ya fedha hizo. Hafla ya kukabidhi mkopo huo imefanyika leo Ijumaa, Februari 28, 2025, chini ya mpango wa asilimia 10 ya makusanyo ya halmashauri, ambapo wanawake wanapewa asilimia nne, vijana asilimia nne na…