Tanzania mbioni matibabu, upasuaji kwa roboti

Dar es Salaam. Tanzania inakaribia kuingia katika teknolojia ya upasuaji kwa kutumia akili mnemba ‘roboti’ baada ya baadhi ya hospitali nchini kuanza maandalizi ya huduma hiyo kwa kutoa mafunzo kwa wataalamu. Hospitali hizo ni pamoja na Taasisi ya Saratani Ocean Road ORCI, Hospitali ya Benjamin Mkapa BMH na Hospitali ya Saifee Tanzania. Desemba 31, 2024…

Read More

Aliyebeba kibuyu tukio la Muungano azikwa, Shoo ataka umakini kwenye elimu

Hai. Wakati Sifael Shuma (92)aliyekuwa mmoja wa vijana wanne walioshiriki tukio la kuchanganya udongo, Aprili 26,1965,akizikwa nyumbani kwake Machame, Wilaya ya Hai, Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Fredrick Shoo ameiomba Serikali kuwekeza katika sekta ya elimu na kuhakikisha wanazalishwa vijana wenye elimu bora.  Dk Shoo amesema…

Read More

Rais Samia na mkakati wa kuifanya Tanga kuwa ufunguo wa uchumi

Pangani. Rais Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Serikali ni kuunganisha Mkoa wa Tanga na shoroba kadhaa ili kufungua biashara, utalii na hatimaye uchumi wa mkoa huo na taifa kwa ujumla. Mkakati wa kuifungua Tanga, kwa mujibu wa mkuu huyo wa nchi, unaanzia wilayani Pangani, ambako unatekelezwa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo (Makurunge)-Mkange-Pangani-Tanga…

Read More

Zanzibar ina mtaalamu mmoja wa upasuaji moyo

Unguja.  Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa wataalamu wa magonjwa ya moyo, ambapo kwa sasa kuna wataalamu wa moyo wanne pekee, huku mmoja tu akiwa na uwezo wa kufanya upasuaji wa moyo. Hali hii imebainika wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Moyo Tanzania (CardioTan 2025) pamoja na mafunzo ya awali ya uokoaji…

Read More

Wananchi 10,270 wapatiwa boti za uvuvi, mwani

Unguja. Wananchi 10,270 wamepatiwa boti za kuendeshea kilimo cha mwani kati ya hao 5,389 vijana, 3,159 wanawake na 1,722 wanaume, boti hizo zimetolewa kupitia programu ya Uviko-19. Pia, kupitia programu hiyo, Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi ilitoa mafunzo kwa wakulima wa mwani 7,300 kuhusiana na namna bora ya kufanya shughuli zao ambao zaidi…

Read More

Ujumbe wa Kwaresima wa Papa Francis kwa 2025

Dar es Salaam. Siku sita kabla ya kuanza kwa kipindi cha Kwaresima mwaka 2025, Papa Francis ametoa ujumbe kwa waumini wa Kanisa Katoliki ukiongozwa na kaulimbiu “Tembeeni pamoja kwa matumaini”, akisisitiza kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma.  Kaulimbiu hiyo inawahimiza waumini kusafiri pamoja kama mahujaji wa matumaini kuelekea nchi ya ahadi, wakihakikisha hakuna anayeachwa au kutengwa,…

Read More