Watu wawili wafariki ajali ya basi na lori Shinyanga
Shinyanga. Madereva wawili wa Fuso na basi aina ya Tata wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea barabara kuu ya Tinde–Isaka, eneo la Tarafa ya Itwangi, Kijiji cha Nyashimbi. Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema chanzo ni uzembe wa dereva wa basi. Amesema ajali hiyo ilitokea Septemba 6, 2025 majira…